Ligi Kuu

Katwila: Malengo ni kubaki Ligi Kuu msimu ujao

GEITA: KOCHA wa Geita Gold, Zuberi Katwila ameeleza kuwa malengo yao kwa sasa ni kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Katwila amesisitiza hayo akibainisha wamerejea Ligi Kuu na kukuta ushindani mkubwa ingawa na wao wamejipanga kuhakikisha wanatoa ushindani wa kutosha.

Mpaka sasa, Geita imecheza mechi tano ambapo imeshinda mbili, sare moja na kufungwa mbili. Inashikilia nafasi ya sita kwa pointi zake saba.

“Nashukuru Mungu tumeanza vizuri kwa maana tumepata matokeo kutokana na maandalizi tuliyojiandaa nayo kwa hiyo sio mbaya kwetu mpaka sasa.

“Malengo makubwa ni kuhakikisha timu inasalia Ligi Kuu msimu ujao maana ushindani tumeukuta ni mkubwa na kila timu imejiandaa, ingawa tunachohitaji zaidi timu pia imalize kwenye nafasi za juu,” alieleza Katwila.

Akizungumzia mchezo wao unaofuata dhidi ya Yanga, Katwila alisema wanaendelea na maandalizi ya kutosha wakifahamu wanakutana na timu bora kwenye ligi.

“Tunajiandaa vya kutosha kwa ajili ya kukutana na Yanga ambao wanaonekana bora na wako vizuri kwa hiyo sasa hivi jicho letu ni mechi inayokuja dhidi ya Yanga, ni miongoni mwa pointi tatu tunazozihitaji ili kujiweka sawa,” alisema Katwila.

Geita itakuwa ugenini katika mchezo huo unaotarajia kupigwa Septemba 15, mwaka huu dimba la KMC Complex, Dar es Salaam majira ya saa 1 jioni.

Related Articles

Back to top button