Ligi Kuu

Simba yawashusha presha mashabiki jeraha la Mutale

DAR ES SALAAM: HATMA ya ukubwa wa jeraha la kiungo mshambuliaji wa Simba, Joshua Mutale kujulikana kesho baada ya kufanyiwa vipimo vya awali vya madaktari.

Joshua alipata jeraha ya nyama za paja katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa Agosti 18, 2024 dhidi ya Tabora United na kutolewa dakika ya 31 ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa KMC , uliopo Mwenge DSM.

Kwa mujibu wa daktari wa Simba, Edwin Kagabo jeraha alilopata kiungo huyo sio kubwa na tayari ameanza kupatiwa matibabu baada ya kuondolewa kwenye mchezo huo.

“Mutale alipata maumivu ya nyama za paja na tayari ameanza matibabu ya awali na uchunguzi kuhusu ukubwa wa tatizo lake utakamilika baada ya saa 48,” amesema daktari huyo wa Simba.

Ameongeza kuwa Mutale amepata changamoto ya nyama za paja Kitaalamu (Hamstring Muscles) lakini hali yake sio mbaya sana na tunatarajia kupata taarifa nzuri ambazo sio za kumuweka nje muda mrefu.

 

Related Articles

Back to top button