Muziki

Mkenya anatamani kuweka historia ya kupuliza Tarumbeta

NAIROBI: MPIGA tarumbeta na mtayarishaji mashuhuri wa muziki nchini Kenya, Mackinlay anatazamiwa kuweka historia kwa jaribio la Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa onesho la muda mrefu zaidi la tarumbeta akipanga kutumia saa 24 akipuliza tarumbeta bila kukoma.Tukio hili lisilo la kawaida litafanyika katika Mkahawa wa Geco jijini Nairobi Januari 31, 2025, kuanzia saa 10:00 jion.

Mackinlay Oktoba 12 mwaka jana alifanya tamasha la kupupiza tarumbeta kwa saa 12 katika ukumbi huo wa Mkahawa wa Geco.

Mackinlay analenga kuhamasisha hadhira duniani kote kwa ujumbe, “Hakuna binadamu aliye na kikomo,” akirejea falsafa ya gwiji wa mbio za marathoni wa Kenya Eliud Kipchoge. “Jaribio hili ni safari ya kujitambua, ushuhuda wa uwezo wa binadamu na fursa ya kuhamasisha wabunifu kusukuma mipaka,”

Mackinlay amesema jaribio hilo la kuvunja rekodi alianza kulipanga miezi sita, iliyopita alihusisha ushirikiano na wanamuziki wenye vipaji huku akiweka programu kali ya mazoezi ya mwili na maandalizi makali ili kuhakikisha anakuwa na ustahimilivu wa muziki na kimwili.

Related Articles

Back to top button