Nyumbani

JKT Queens yaendeleza ubabe GIFT

DAR ES SALAAM: TIMU ya JKT Queens imeendelea kufanya vizuri kwenye mchezo wa pili mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya  Kenya Elite Junior Academy, Ukiwa mchezo wa pili wa JKT Queens kwenye michuano ‘U17 Girls Integrated Football Tournament’ (GIFT) uliochezwa  uwanja Azam Complex Chamazi Dar es Salaam.

Mabao ya JKT Queens yamefungwa na Lidya Kabambo dakika ya 30 pasi kutoka kwa Yasinta Mitoga.
Bao la pili limefungwa na Adija Sanyenge dakika ya 60. Kenya Elite Junior Academy imepata bao la kwanza la kujifunga na beki wa JKT Queens, Furaha Kifaru dakika ya 65.

Huu ni ushindi  wa pili wa JKT Queens baada ya mechi ya kwanza ya ufunguzi kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya K.A.S

Related Articles

Back to top button