Kwingineko
Infantino minne tena FIFA

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) Gianni Infantino amechaguliwa kuendelea na wadhifa huo kwa muhula wa ofisi 2023-2027.
Amechaguliwa bila kupingwa katika mkutano wa 73 wa FIFA uliofanyika Kigali, Rwanda.
““Kuwa rais wa FIFA ni heshima na fursa kubwa lakini pia ni jukumu kubwa,” amesema Infantino.
Hiyo ni mara ya nne kwa mkutano wa FIFA kufanyika barani Afrika.