BurudaniMuziki

Harmonize aiteka Bongo

DAR ES SALAAM; Msanii wa na Bongo fleva Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ amewasili nchini akitokea Marekani alikoshinda Tuzo tatu za AEAUSA ambazo ni msanii bora wa mwaka 2023 (Artist of the year 2023),Video bora ya mwaka (Best Music Video,single again’) na King of The East and Bongo Afro Bongo Flavour.
Mara baada ya kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, msanii huyo amepokelewa kwa furaha na Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Dk. Kedmon Mapana pamoja na viongozi wengine wa BASATA.
Waandishi wa habari na Mashabiki wake wamejitokeza kwa wingi katika kumpokea msanii huyo.
Katibu Mtendaji wa Basata Tanzania, Dk Kedmon Mapana ameziwasilisha salamu za Pongezi kwa Harmonize kutoka kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Related Articles

Back to top button