Hakuna kulala!
DAR ES SALAAM: BEKI wa Yanga Kibwana Shomary amesema kwa namna yoyote ile lazima msimu huu ahakikishe anapata muda mwingi wa kucheza katakana kikosi chao na kuisaidia timu.
Kibwana ameitumikia Yanga kwa misimu minne na hivi karibuni aliongezewa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu ya Wananchi kwa miaka miwili mbele, msimu uliopita hakupata muda mwingi wa kuchezwa na kumpisha mpinzani wake kwenye namba katika kikosi cha Yanga Kouassi Yao, kupata nafasi zaidi.
Amesema anatarajia kufanya vizuri msimu mpya utakapoanza na kuendelea kukusanya mataji kwa sababu ya usajili uliofanywa kwa kuboresha baadhi ya nafasi na kuwa timu imara zaidi ya msimu uliopita.
“Kazini kwangu kuna kazi kutokana na ushindani uliopo, lakini nadhani huu ni muda sahihi kwangu kupambana kwa nguvu zote ili msimu ujao nipata muda mwingi wa kucheza na kuisaidia timu kufikia malengo.
Wananchi wameniamini na kunipa muda mwingine wa kuitumikia nami lazima nionyeshe kuwa hawakufanya makosa kwa kuwatumikia kwa nguvu na kuendelea kuwapa furaha mashabiki wetu ” amesema Kibwana.
Ameongeza kuwa wachezaji wapya wamepewa maelekezo na mikakati ya timu kubwa ni kuchukuwa makombe, nao wanatakiaa kupambana na kujitoa kusaidiana ili kufikia ma lengo hayo.