Habari Mpya

Guardiola ashangazwa na Haaland

MANCHESTER: Kocha mkuu wa Wababe wa ligi kuu ya England Manchester city Pep Guardiola amesema anashangazwa na uwezo mkubwa wa mshambuliaji wake Erling Haaland msimu huu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Inter Milan hapo kesho Pep amesema anashangazwa na uwezo mkubwa wa kufunga wa kinara huyo wa mabao wa ligi kuu ya England mpaka sasa

Hiyo inakuja baada ya mwandishi mmoja wa habari kutaka kujua kama meneja huyo wa Manchester city anashangazwa na takwimu za Erling Haaland.

“Kidogo, ndio. unajua kwa nini? Nilicheza soka miaka 11 na nilifunga mabao 11 tu, Jamaa huyu katika mechi nne tayari amefunga mabao tisa, wewe unaona kawaida?” amesema Guardiola

Haaland amekuwa chaguo la kwanza la Pep Guardiola tangu alipotua kikosini hapo akitokea Borussia Dortmund na msimu huu tayari amefunga mabao 9 katika michezo 4 ya ligi kuu ya England.

Katika ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu uliopita Haaland alimaliza akiwa na mabao 6 huku akiwa na jumla ya mabao 41 katika michezo 39 ya ligi hiyo tangu aanze kucheza

Related Articles

Back to top button