Habari Mpya

Dube anawataka leo, kesho

AFRIKA KUSINI: MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Prince Dube amesema kuwa tabu kwa wapinzani wao iko palepale kwani amejipanga kuisaidia timu yake hiyo kufanikiwa kufanya vizuri kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii na mashindano mengine ya msimu wa 2024/25.

Dube anaweza kuwa ndio mchezaji aliyeifunga Simba mara nyingi kuliko wote wakati akiwatumikia wana lambalamba Azam FC na wanakutana nao katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 8, mwaka huu uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam

Mchezaji huyo amesajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao na kwa mara nyingine anaenda kukutana na Simba na safari akiwa na jezi yenye rangi ya Kijani na Njano.

Dube amesema hana wasiwasi na mechi hiyo kwa sababu anafahamu uwezo wake wa kufunga katika eneo ambalo mabeki na makipa hawatarajii.

“Nimekuwa nikifunga dhidi ya Simba kila nikikutana nao, nimekutana na wachezaji bora na wazuri, ninaimani ya kufanya vizuri katika mchezo huo kushirikiana na wachezaji wenzangu kufikia malengo yanayotarajiwa na Wananchi,” amesema Dube.

Ameongeza wanajiandaa vizuri na anaimani msimu ujao utakuwa bora kwa sababu ya ubora wa wachezaji waliokuwepo ndani ya timu hiyo.

Dube ni mshambuliaji wa pili wa usajili mpya waliyefanikiwa kufunga bao katika michezo miwili ya kirafiki alifunga katika mechi ya TS Gallaxy na Jean Baleke aliyeanza kufunga katika mchezo wa kwanza na FC Augsburg.

Related Articles

Back to top button