EPL

Guardiola alia na majeraha Man City

LONDON: Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester City Pep Guardiola amesema wingi wa majeruhi katika kikosi chake unampa wakati mgumu hasa wakati huu ambao inamlazimu kufanya ‘rotation’ ya kikosi kutokana na wingi wa mechi.

Guardiola amesema Manchester City ina wachezaji 13 pekee walio kamili kucheza akitaja jambo hilo kama jambo linalomtatiza zaidi kwa sasa.

“Ndio tuna wachezaji 13 tu walio tayari kucheza, wengi wao waliocheza hivi majuzi walimaliza na matatizo. Nadhani tuko kwenye kipindi kigumu sana kwa sababu kwa miaka 9 hatujawahi kuwa na majeruhi wengi hivi” amesema.

Manchester City wameondoshwa kwenye michuano ya kombe la Carabao kwa kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspur waliokuwa nyumbani dimba la Tottenham Hotspur stadium jijini London

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button