EPLKwingineko

Etihad kufikisha watazamaji Elfu-60

KLABU ya Manchester City imewasilisha maombi ya mpango wa kupanua uwanja wake wa Etihad kwa gharama ya pauni milioni 300 sawa na shilingi bilioni 865.49.

Timu hiyo inataka kuongeza idadi ya mashabiki kwenye uwanja huo kutoka wa sasa 53,400 hadi 60,000 kwa kupanua jukwaa la Kaskazini.

Mapendekezo hayo yanajumuisha eneo la baa linalotazamana na sehemu ya kuchezea na eneo la kufunuka uwanja.

Eneo la mashabiki 3000, duka jipya la klabu na makumbusho na hoteli yenye vyumba 400 pia vimependekezwa katika maombi hayo yaliyotumwa Halmashauri ya Jiji la Manchester.

Klabu hiyo imesema mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu utakuwa wa daraja la juu na kuleta burudani kwa mashabiki mwaka mzima.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button