Filamu

Filamu ya ‘Spider-Man 4’ kuachiwa Julai 24, 2026

NEW YORK : Filamu ya ‘Spider Man 4’ inayoigizwa na Tom Holland kama muigizaji mkuu itaanza kurekodiwa msimu ujao wa joto na inatarajiwa kuachiwa sokoni Julai 24, 2026, Sony imetangaza.

Erik Sommers na Chris McKenna, ambaye aliandika ‘Spider-Man: No Way Home’ ya 2021 wameiandika filamu hiyo itakayoongozwa na Destin Daniel Cretton.

Filamu hiyo itatolewa wiki moja baada ya filamu inayofuata ya Christopher Nolan, ambayo pia ataigiza mkali huyo wa Spider Man, Tom Holland.

Holland hapo awali alikiri kuwa alikuwa amejiandikisha kwa filamu inayofuata ya Nolan bila kujua inahusu nini?

Akiongea kwenye ‘Good Morning America’: “Ninachoweza kusema ni kwamba nimefurahia sana … lakini hiyo ndiyo tu ninaweza kusema kwa sababu, hiyo ndiyo ninayojua lakini mradi wa Nolan ni mradi mzuri kwangu kimaisha licha ya kusahini bila kuujua.”

Holland alikiri kupokea simu kuhusu mradi ujao wa Nolan ilimkumbusha kujisajili kuwa nyota kama Peter Park/ Spider-Man, ambaye tayari ameigiza katika filamu sita.

Alisema: “Fursa ilipopatikana, ilikuwa simu ya maisha. Ilikuwa ni ukumbusho wa kupata simu kuhusu ‘Spider-Man’ miaka 10 iliyopita. Ni jambo la kushangaza kwangu. Ninajivunia sana na ninafurahia sana.”

Wakati huo huo, Tom hivi majuzi alifichua kuwa yeye na mpenzi wake Zendaya – ambaye anaigiza mwenzi wa Peter Parker MJ katika filamu za ‘Spider-Man’ – walikuwa wanarukaruka chumbani kwa msisimko baada ya kusoma mswada wa kwanza wa ‘Spider-Man 4’.

Related Articles

Back to top button