Filamu

Filamu ya Rebel Ridge yaongoza kutazamwa zaidi nchi 70

FILAMU ya Rebel Ridge imeelezwa kuwa na msisimko mno kwa watazamaji kiasi kwamba inaongoza kwa kutazamwa zaidi katika nchi 71 duniani kote.

Filamu hiyo kwenye mtandao pia imeongoza kwa kutazamwa zaidi kwenye Netflix ambapo imetazamwa mara 31,000,000 katika siku tatu za kwanza kwenye Netflix.

Filamu hiyo kwa sasa ndiyo maarufu zaidi kwenye mtandao huo ikidaiwa kushawishi watu wengi zaidi kuendelea kuitazama filamu hiyo.

Sinema ya ‘Rebel Ridge’ ni filamu ya mapigano ikisaidiwa na mtayarishaji filamu Jeremy Saulnier ikiwa na nyota Aaron Pierre kama Terry Richmond, mwanajeshi wa zamani ambaye anajitokeza dhidi ya mkuu wa polisi wa Marekani fisadi anapojaribu kumtoa gerezani binamu yake asiye na hatia.

Nyota wa filamu hiyo Pierre alifichua kwamba filamu hiyo mpya ilikuwa imeshika nafasi ya kwanza katika zaidi ya nchi 70 ikiwa ni pamoja na Uingereza.

‘#1 kwenye Netflix katika nchi 71 tofauti! Lo! Moyo wangu umejaa,’ alichapisha mwigizaji huyo wa Uingereza mwenye miaka 30 kwenye ukuras wake wa Instagram.

‘Hili lisingewezekana bila wewe. Huu ni ushindi wa timu. Asanteni nyote kwa upendo na nguvu nzuri,’ aliendelea. ‘Asante kwa kila mtu ambaye alijimiminia katika kutengeneza Rebel Ridge,” alieleza kwa furaha.

Katika filamu hiyo nyota wa Hollywood Don Johnson amecheza pamoja na Chief Sandy Burnne na Anna Sophia Robb, David Denman, Emory Cohen na James Cromwell.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button