Nyoka asitisha upigaji picha za filamu

EQUADOR
MUONGOZAJI wa filamu, Ron Howard amelazimika kusitisha kurekodi filamu yake mpya ili nyoka waweze kuondolewa eneo walilokwa wameandaa kwa ajili ya upigaji picha za sinema yake ndipo waendelee na kazi hiyo.
Mtayarishaji huyo mwenye umri wa miaka 70 aliajiri wataalamu wa wanyama kuwakamata wanyama hao waliohofiwa kuwa na sumu na kuwatoa eneo hilo ili wasiwadhuru waigizaji wengine.
Filamu hiyo yenye hadithi ya Vita vya Kwanza vya Kidunia ilikuwa ikirekodiwa kwenye Visiwa vya Galapagos.
Ron alisema “Tunawaondoa Wanyama hao ili risasi zilizokuwa zikipigwa katika uandaaji wa filamu hizo zisiwaguse na pia waigizaji wangu wasipate madhara kutoka kwa nyoka hao,”.
Hata hivyo baada ya kutolewa nyoka hao baadhi ya wasanii walitaka kuendelea na wengine kulala hapo hapo bila kujali nyoka hao lakini mwandaaji wa filamu hiyo alikataa ili kutowaweka katika hatari ya Wanyama wenye sumu.
Howard alisema maandalizi ya filamu hiyo ya ‘Edeni’ yalikuwa yamekamilika lakini nyoka hao na wadudu wataambaao wanaohisiwa kuwa na sumu kali ndiyo walikuwa kikwazi katika upigaji picha za sinema hiyo.