Fadlu:Nahitaji alama 10 shirikisho

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema malengo yake ni kutafuta alama 10 katika michezo ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika.
Fadlu ameliambia Spotileo kuwa mechi za hatua ya makundi zitakuwa ngumu lakini wanajiandaa kutafuta pointi kila mechi ili kuweza kufuzu hatua inayofuata.
“Malengo yetu ni kutafuta pointi 10 au zaidi, tunatakiwa kushinda mechi za nyumbani zote tatu na ugenini kutafuta alama muhimu ikiwemo zote tatu au moja ili kujihakikishia kufuzu,” amesema Kocha huyo.
Jumatatu Oktoba 7, droo imepangwa nchini Misri ambapo wawakilishi kwenye anga hilo kutoka Tanzania ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Simba imepangwa kundi A ikiwa na timu za CS Sfaxien (Tunisia), CS Constantine (Algeria) na FC Bravos do Maquis (Angola).