
KIKOSI cha timu ya Yanga kimewasili jijini Mwanza tayari kuikabili Geita Gold katika mfululizo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
Timu hizo zitavaana Oktoba 29 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Yanga inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 17 baada ya michezo 7 wakati Geita Gold ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 9.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu utakaofanyika Oktoba 29 utazikutanisha Tanzania Prisons na Namungo katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika mchezo mmoja uliopigwa Oktoba 27 wekundu wa Msimbazi, Simba ilijikuta ikipoteza mchezo wa kwanza wa ligi kuu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.