Chasambi: Tulieni niwape vitu
DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Simba, Ladack Chasambi amesema ataendelea kupambana kwenye uwanja wa mazoezi ili apate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza chini ya Kocha Fadlu David.
Chasambi ni moja ya wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kucheza tangu kuanza kwa msimu huu, ameweka wazi kwamba anataka kuja kivingine kuwapa fuaraha mashabiki wa Simba.
Amesema kupata nafasi ya kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ni juhudu ambayo amekuwa akionesha mazoezini kilichofanya kocha Fadlu kumuamini katika kikosi cha timu yake.
“Nilicheza kwa kufuata maelekezo ya kocha Fadlu na maandalizi mazuri ambayo nilifanya,nashukuru niliweza kufanya vizuri na nitahakikisha ninaendelea kufanya vizuri na kusaidia timu kupata matokeo mazuri katika michezo inayokuja,” amesema.
Chasambi amefunguka kwamba kabla ya mechi kocha Fadlu alizungumza naye na kumtia nguvu kuwa afanye vizuri kama ilivyokuwa mazoezini, asiwe muoga akioneshe alichokuwa nacho mguuni.
“Nilifuata maneno yake kwa sababu sijacheza muda mrefu, nilifanikiwa kufuata maelekezo nawaahidi mashabiki kupambana kusaidia timu kupata matokeo chanya kwa kila mechi,” amesema Chasambi.