Tetesi

Eze kulamba mil 303/- kwa wiki

TETESI za usajili zinasema fowadi wa England, Eberechi Eze mwenye umri wa miaka 25 anakaribia kusaini mkataba mpya Crystal Palace wa pauni 100,000 sawa shs milioni 303.2 kwa wiki baada ya kukubali dili kimsingi.(Mail)

Fowadi wa England Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kuondoka Manchester United Januari 2024.(Fabrizio Romano)

Chelsea na Liverpool zimeonesha nia kumsajili fowadi wa kihispania wa klabu ya Real Betis mwenye umri wa miaka 18, Assane Diao, Januari 2024.(Fichajes – in Spanish)

Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta, huenda akawauza wachezaji wanne Januari 2024 ili kupata fedha zinazohitajika kumsajili mshambuliaji wa Brentford na England mwenye umri wa miaka 27, Ivan Toney.(Athletic, via Express)

Real Madrid haina mpango wa kumsajili fowadi Kylian Mbappe hata kama hataongeza mkataba wake Paris Saint-Germain na kuondoka akiwa huru majira yajayo ya kiangazi.(Cadena SER – in Spanish)

Related Articles

Back to top button