Tetesi

Potter njia moja West Ham

LONDON:MENEJA wa zamani wa Chelsea Graham Potter yuko mbioni kujiunga na wagonga nyundo wa London West Ham united baada ya pande hizo mbili kupiga hatua katika mazungumzo ya mkataba.

Kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England kimeripoti kuwepo kwa nia ya dhati ya pande hizo kufanikisha mkataba wa meneja huyo mwenye miaka 49 kuanza mara moja kazi ya kuwanoa wagonga nyundo hao.

Ikiwa dili hili litatiki Potter ataiongoza West Ham kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi Aston Villa dimbani Villa Park ijumaa ya Januari 10 na klabu hiyo imeahirisha mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo kwa kile kinachotajwa kuandaliwa kwa Potter kutwaa nafasi hiyo.

West Ham united imeshinda mchezo mmoja tu kati ya mechi 5 zilizopita ikitoa sare mbili na vipigo viwili vizito vya bao 5 kutoka kwa Liverpool na bao 4 kutoka kwa Manchester City.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button