NyumbaniTetesiWasifu

Kauli hii ya Karia itawagusa wengi

atoa maagizo kwa klabu ligi kuu

KIGOMA: KLABU za Ligi Kuu Tanzania Bara zimetakiwa kumiliki viwanja vya mazoezi kabla ya msimu ujao kulingana na vigezo vya leseni za klabu .

Rais wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema hayo leo katika mkutano mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara unaoendelea mkoani Kigoma ambapo amesema klabu zinazoshiriki ligi kuu zinatakiwa kumiliki viwanja vyao vya kufanyia mazoezi.

“Msimu ujao sitaki tena kuona klabu ina kodi au kuomba uwanja wa mazoezi kama haitafuata maelekezo, imeondoka kwenye vigezo watakuwa nje ya klabu License,” amesema.

Karia amesema kuhusu uwanja wa kuchezea bado wanashirikiana na Serikali kwa ajili ya kufanya ukarabati na utengenezaji wa  viwanja bora ili kuepuka kufungia viwanja.

“Tukumbuke kuwa ligi yetu inashika nafasi ya sita kwenye ubora Afrika kuepuka kushuka kwenye hiyo nafasi tunangalia kila mkoa kuwa na kiwango kizuri kwa ajili ya mechi,” amesema Karia.

Related Articles

Back to top button