Habari Mpya
EURO 2024 : Mfaransa kuamua vita ya Spain na Egland

BERLIN: Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limwemteua Mfaransa François Letexier kusimamia sheria 17 za soka kwenye mchezo wa fainali ya EURO2024 itakayopigwa katika dimba la Olympiastadion jijini Berlin.
Refa huyo mwenye miaka 35 amekuwa mwamuzi wa kati tangu mwaka 2017 akichezesha michezo 65 inayosimamiwa na UEFA
Katika michuano hii Letexier amechezesha mechi baina ya Spain vs Georgia hatua ya 16 bora na mechi mbili za hatua ya makundi za Croatia vs Albania na Denmark vs Serbia pia amekuwa mwamuzi wa akiba katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo baina ya wenyeji Germany na Scotland