Habari Mpya

Kisa cha Komphela kuwadengulia Simba hiki hapa

Hatimaye imebainika sababu ya Kocha Steve Komphela kuidengulia Simba licha ya kuingia makubaliano ya awali ya kuja kukionoa kikosi hicho kwa msimu ujao.

Spotileo inafahamu kuwa kocha huyo alikwisha kukubaliana kila kitu na Simba na ilikuwa imebaki tuu kutambulishwa rasmi lakini mambo yalibadilika ghafla licha ya kwamba kocha huyo alifika mpka Dar es Salaam akiwa tayari kwa kibarua hicho.

Mapema leo ukweli juu ya Kocha Steve kubadili gia angani umefahamika baada ya kocha huyo kutangazwa kuwa kocha wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyomfuta kazi kocha Rhulani Mokwena siku chache zilizopita.

Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya Mamelodi na kocha Komphela yalianza wakati kocha huyo akikaribia kumalizana na Simba na hapo ndipo alipoanza kubadilika kama kinyonga kwenye dili la Simba na mwisho wa siku akaichomolea kabisa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya msimbazi Dar es Salaam.

Hata hivyo tayari kila mtu amekula Hamsini zake baada ya jana usiku Simba kumtangaza aliyekuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca, Fadlu David kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho kwa mkataba wa miaka miwili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button