Diddy agoma kula Jela kwa hofu ya sumu
NEWYORK: RAPA na mjasiriamali wa Marekani, Sean Combs maarufu P. Diddy ameripotiwa kuanzisha mgomo wa kula kutokana na kuhofia kulishwa sumu.
Kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha Metropolitan (MDC), Diddy anasemekana anahofia kuhusu usalama wake, kulingana na Larry Levine, mfungwa wa zamani anayefahamu kituo hicho.
Combs anadaiwa kuwa na wasiwasi kwamba mtu anaweza kuweka chakula chake sumu na kusababisha mshtuko katika moyo wake.
Diddy alinyimwa dhamana kufuatia kukamatwa kwake Manhattan kwa tuhuma za ulanguzi wa ngono, ulaghai na kusafirisha watu kwa ukahaba.
Wenye mamlaka pia walimpokonya dawa za kulevya, silaha na vitu vingine wakati wa uvamizi nyumbani kwake.
Wakili wa Diddy, Marc Agnifilo, anasisitiza kuwa rapa huyo hataki kujiua. Agnifilo pia ameomba uhamisho wa mteja wake hadi kituo cha New Jersey, ambacho kwa sasa kinakaguliwa na mahakama.