Mastaa

Tangazo la Harusi la Ini Edo lazua taharuki kwa mashabiki wake

NIGERIA: NYOTA wa filamu kutoka nchini Nigeria, Ini Edo ametangaza kufunga ndoa mwaka huu 2024 baada ya kutokuwa katika uhusiano rasmi tangu mwaka 2014 alipoachana na aliyekuwa mume wake, Philip Ehiagwina.

Ini Edo alifunga ndoa na mfanyabiashara Mnigeria mwenye makazi yake nchini Marekani, Philip Ehiagwina, Novemba 29,2008 nchini Marekani lakini walitalikiana mwaka 2014.

Katika chapisho lake katika ukurasa wake wa Instagram nyota huyo wa filamu mwenye umri wa miaka 42 aliweka picha akiwa amevalia vazi la kitamaduni la harusi la Efik. Na maelezo aliyoandika yalionyesha wazi kwamba harusi yake inakaribia ndani ya mwaka huu kwa kuwa amechumbiwa miezi mitatu iliyopita.

Chapisho lake liliwasihi watu wasikate tamaa katika kutafuta furaha huku akisema kwamba mapenzi yangewapata:

“…Asubuhi ya miezi sita iliyopita, tukiwa likizoni, tulivuka njia na maisha yetu hayakubaki vile vile. Miezi mitatu baadaye, uliniuliza niwe nawe milele. Nilipataje bahati hivyo? Wanasema, ‘Kasoro zako ni kamili kwa ajili ya moyo uliokusudiwa kukupenda.’ Sasa ninaamini hili kwa moyo wote. Moja ya tatu kufanyika.

“Harusi yangu ya hadithi inakaribia. Kwa mtu yeyote huko nje ambaye amekata tamaa kwa furaha siku zote na itakapopatikana, tayari au la, litakuwa jambo bora zaidi kuwahi kutokea kwako,” aliandika Ini Edo.

Mashabiki wa mwigizaji huyo walimpongeza muigizaji huyo katika ukurasa wake wa Instagram lakini walishangazwa wakati wa onyesho la Big Brother Naija la kuwahamisha, Biggie na mtangazaji wa kipindi hicho, Ebuka, ambapo Bibi harusi alionekana jukwaani akilia, jambo ambalo liliwachanganya watazamaji zaidi.

Walakini, kwa dakika chache, Ebuka alirejea na kueleza kwamba chapisho la Instagram la Ini lililenga hicho kilichoonyeshwa hapo na kwamba Bibi Harusi analia ilikuwa sehemu ya mfululizo mpya wa sehemu nne ulioigizwa na Ini Edo.

Hata hivyo Ini Edo pia alifichua kuwa mfululizo huo wa Harus Yangu utaanza kuonyeshwa 20Oktoba,2024 wiki tatu baada ya BBNaija kumalizika.

Related Articles

Back to top button