Burudani

Anjella aomba msaada wa matibabu

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo Fleva, Angelina Samson maarufu kama Anjella, ameomba msaada wa matibabu kutokana na changamoto ya kiafya inayomkabili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Anjella ameeleza kuwa amekuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya mguu kwa muda mrefu, hali iliyomfanya kukata tamaa baada ya juhudi zake za kupata nafuu kugonga mwamba.

Amefafanua kuwa licha ya kutumia dawa nyingi, bado hajapata nafuu, na gharama za matibabu yake ni zaidi ya shilingi milioni 13 , kiwango ambacho hawezi kumudu peke yake.

Anjella amesema kuwa amekuwa akialikwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya michezo kama marathoni, lakini kutokana na hali yake ya kiafya, hawezi kushiriki. Ameomba msaada kutoka kwa Watanzania ili aweze kugharamia matibabu yake na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Kwa wale wanaotaka kujua zaidi kuhusu hali ya Anjella na jinsi ya kumsaidia, unaweza kutembelea mtandao wake wa instagramu

Related Articles

Back to top button