Tuzo za Kimataifa za ‘HAP’ kutolewa Agosti 10
TUZO za Kimataifa zinazojulikana kama ‘Hap Awards’ zinatarajia kutolewa nchini Tanzania katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Agosti 10, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kedmon Mapana amesema kuwa tuzo hizi zimegawanywa kwenye vipengele vikuu vitatu.
“Kutakuwa na vipengele vya Muziki, Mitindo na Filamu ambapo tuzo hizo zitatolewa katika usiku huo. Kipengele cha Muziki watashindanishwa wasanii wa muziki wa dansi, singeli, taarabu pamoja na ngoma za asili.” Amesema Mapana.
“Majaji watakuwepo kutoka nchini Marekani na wengine kutoka hapa nchini Tanzania, ambao watakuwa wakifanya mchujo katika vipengele hivyo hadi kupata mshindi. Kutakuwa na Vipengele vya Muziki 11, vipengele 21 vya fasheni pamoja na vipengele 11 vya filamu.”amesema Mapana
Kwa upande wake Mrisho Mrisho ametangaza vipengele vya Muziki wa Bongo fleva, huku watakaochuana katika mitindo ni Asia Idorus pamoja na Mustafa Hassanali.
Wasanii chipukizi kwenye muziki wa Bongo fleva watakaoshindana katika kipengele cha ‘msanii chipukizi’ ni Yammi , Vannillah , Founder Tz, Mrs Energy na Aslam TZ.
Kwa upande wa muziki wa Singeli, watakaoshiriki ni Dulla Makabila, D Voice, Sholo Mwamba, Meja Kunta na Yamoto Band.
Kwa upande wa muziki wa Injili washindani ni Zabron Singers, Neema Gospel Choir, Agape Gospel Band, Joel Lwaga na Rose Mhando