Burudani

Njooni mcheke kisomi

DAR ES SALAAM: Wanafunzi wa vyuo mbalimbali wametakiwa kujitokeza kwenye Shindano la kusaka Vipaji vya Comedy lililopewa jina la Cheka Kisomi linalotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa cheka kisomi Caroline Raymond Nkya leo amesema rasmi yameanza mashindano ya kusaka vipaji vya kuchekesha ‘stand up comed’ haswa vyuoni mashindano hayo yataanza Mkoa wa Dar es Salaam.

“Sanaa ni ajira na kuna nafasi ya kujiajiri kwa namba mbalimbali hii ni fursa kwa wanavyuo wanaojua na kuona wanakipaji cha kuchekesha waweze kujitokeza.”

“Mashindano aya tunasisitiza kuwa sanaa si burudani pekee bali tunahitaji taaluma ambayo ni elimu au ujuzi ili kufanikiwa malengo ya mtu anayechekesha zaidi” Caroline

Pia ameongeza kuwa lengo kuu ni kukuza elimu ya sanaa ya uchekeshaji kuwaunganisha vijana na fursa mbalimbali ikiwemo kushiriki katika matamasha makubwa ya uchekeshaji hapa nchini.

Related Articles

Back to top button