
BAADA ya maneno kuwa mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuyumba kwa ndoa ya msanii wa filamu nchini Jacquline Wolper amewajia juu wanaosema ameachwa, mwanadada huyo amesema hajaachwa na mume wake bado wapo na ndoa yao hadi kifo kiwatenganishe.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Wolper amesema kuwa watu wanashindwa kujua kuna kufa na kuzikana hawezi kuachika kwa maneno ya watu labda atakapotaka yeye mwenye kuachika.
“Siachwi siwezi kuachwa labda nikitaka mwenyewe na kama baba P aitwe aje kusema hapa kama anauwezo wa kuniacha kama anawadanganya michepuko kaniacha hawezi hana uwezo ikitokea nimeshindwa ndoa nitakuja kuwatangazia kwenye mitandao kuwa nimeacha tutalea watoto.”amasema Wolper
Pia amesema kuwa watu wamuache na maisha yake kwani hapendi kufatiliwa.