EPL

De Zebri akerwa na sare dhidi ya Leeds

LONDON: KOCHA Mkuu wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi ameonesha wazi kukerwa baada ya timu yake kushindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Leeds United kufuatia sare ya 1-1 iliyozidi kuiweka Spurs kwenye presha ya kushuka daraja katika Ligi Kuu England.

Spurs walitangulia kupitia bao kali la Mathys Tel kabla ya makosa ya nyota huyo huyo kuigharimu timu hiyo baada ya kusababisha penalti iliyofungwa na Dominic Calvert-Lewin na kuipa Leeds pointi muhimu ugenini.

Matokeo hayo yanaifanya Spurs kuendelea kubaki kwenye hatari ya kushuka daraja huku ikiwa imebakiza michezo miwili pekee kabla ya msimu kumalizika.

De Zerbi amesema timu yake imeathiriwa na presha ya mapambano ya kubaki Ligi Kuu lakini bado anaamini wachezaji wake wana morali nzuri ya kupambana hadi mwisho wa msimu.

Kipa Antonin Kinsky alikuwa shujaa kwa Spurs baada ya kuokoa michomo miwili muhimu iliyoiwezesha timu hiyo kupata angalau pointi moja nyumbani.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button