Dar City ni mwendo wa ushindi Kenya

MWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kanda ya tano Afrika Mashariki (EABGC) Dar City imeshinda mchezo wa pili baada ya kuichakaza KPA ya Kenya kwa pointi 69-65.
Huo ni mchezo wa pili mfululizo ikitoka kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Equity ya Kenya kwa pointi 83-64.
Msemaji wa Dar City Revocatus Chipando ‘Baba Levo’ amesema Dar City bado iko mikono salama akitamba kuwa ni mwendo wa ushindi.
“Asante Mungu, asante Rais Samia kwa mara nyingine tunawapiga wakenya. Dar City iko kwenye mikono salama, tunaifanya Kenya tunavyotaka,”amesema.
Michuano hiyo ilianza juzi na itaendelea hadi Jumamosi ya wiki hii kutafuta bingwa atakayeenda hatua nyingine za michuano hiyo kuwania nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika.
Bado kuna kibarua Kizito mbele dhidi ya Les Hipos, Remesha za Burundi na ABC ya Tanzania kuelekea kusaka nafasi ya kusonga mbele hatua nyingine ya michuano hiyo ya Afrika.