Chelsea yang’ang’ana na Acheampong

LONDON, ENGLAND: Wababe wa jiji la London Chelsea wamemuongezea beki wake wa kulia Josh Acheampong mkataba mpya wa miaka mitano ambao utamuweka klabuni hapo hapo mpaka 2030.
Kusaini huku mkataba kwa beki huyo Mwingereza kunahitimisha uvumi juu ya hatma yake klabuni hapo baada ya mchezaji na klabu yake hiyo kukubaliana kuboreshwa kwa mkataba wake.
Baada ya kucheza kwa dakika chache kwenye mechi ya kombe la Carabao mwanzoni mwa msimu huu, kinda huyo aliwekwa kando baada ya kukataa majadiliano ya mkataba mpya.
Vigogo Liverpool, Real Madrid and Bayern Munich walitajwa kuwania saini ya beki huyo kiraka ambaye mkataba wake wa sasa ungemalizika katikati ya msimu ujao
Lakini mazungumzo yenye tija ya kuongeza mkataba wa beki huyo yalifanyika katikati ya mwezi uliopita, ikashuhudiwa Acheampong akirejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza cha Chelsea.
Kinda huyo alikanyaga boli kwa dakika 90 akiwa sehemu ya kikosi kilichoibugiza Astana mabao 3-1 kwenye Conference League Alhamisi iliyopita.