Kwingineko

Chande ahimiza kampuni za bima kugeukia michezo

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Wizara ya fedha Hamad Hassan Chande amezungumzia umuhimu wa kampuni za bima kugeukia fursa zilizopo kwenye sekta ya michezo.

Chande amesema hayo Dar es Salaam Jana usiku kwenye uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa soko la bima kwa mwaka 2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa bima Tanzania (TIRA).

Amesema michezo ni sekta inayokuwa hivyo ni vyema ukafanyima utafiti ili kuona namna bora ya kuwafikia wadau wa michezo.

“Kampuni za bima fanyeni utafiti ili vijana na wao wawe na bima rasmi kwenye michezo,”amesema.

Chande pia, ametoa pongezi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Benki ya Biashara ya NBC ambao ni wadhamini wakuu wa Ligi Kuu kwa kuanzisha mchakato wa mazungumzo na baadhi ya makampuni ya bima na kuingia nao mikataba na kampuni hizo.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani sekta ya michezo imekua ikifanya vizuri akitolea mfano timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ imefuzu mara mbili kushiriki fainali za Afrika na kumpongeza pia kwa kutoa bonasi ya sh milioni 700 kwa wachezaji.

Related Articles

Back to top button