EPL

Calafiori ampa kiwewe Arteta

LONDON: KOCHA wa Washika mitutu wa jiji la London Arsenal Mikel Arteta ameonesha wasiwasi juu ya uwezekano wa kumkosa beki wake kitasa Ricardo Calafiori aliyepata majeraha kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Arsenal ikishinda 1-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk.

Calafiori ambaye nafasi yake ilichukuliwa na beki wa kizazi kipya Myles Lewis-Skelly, ni mchezaji wa karibuni zaidi kupata majeraha na anaongezeka kwenye orodha ndefu ya wachezaji ambao wataukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya vinara wa ligi ya England, Liverpool.

“Ililazimu atoke kwa sababu alihisi maumivu, Sijui ukubwa wa tatizo lake hivyo hii sio habari njema.” Alisema Arteta baada ya mchezo wa Jumanne usiku

Arsenal watamkosa pia William Saliba katika safu ya ulinzi kwa kufungiwa baada ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya Bournemouth, huku Jurrien Timber hajaonekana uwanjani tangu mwanzo wa mwezi huu kutokana na jeraha.

Kikosi cha Arteta pia hakitakuwa na mabeki Takehiro Tomiyasu na Kieran Tierney kutokana na majeraha ya muda mrefu.

Martin Odegaard bado hajarejea, wakati huo huo Bukayo Saka amekosa mechi mbili zilizopita kutokana na tatizo la misuli ya paja, alilolipata akiwa na timu ya taifa ya England.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button