Ligi Kuu

Barker, Depu wang’ara Februari

De Reuck, Nado chali

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker, amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2025/2026.

Aidha, Mshambuliaji wa Yanga, Laurindo Aurelio ‘Depu’ amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2025/2026,

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi yq Ligi Kuu,Barker, aliyeingia fainali na Pedro Goncalves wa Yanga na Florent Ibenge wa Azam, aliweza kuiongoza timu yake kushinda michezo miwili na kutoka sare moja, jambo lililomsaidia kupanda kutoka nafasi ya sita hadi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji wa Yanga, Laurindo Aurelio ‘Depu’ amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2025/2026,

Laurindo alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo kwa mwezi huo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili katika michezo miwili ambayo Yanga ilicheza, na kuisaidia timu yake kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

Mshambuliaji huyo amewashinda beki Rushine De Reuck wa Simba na kiungo Ida Selemani ‘Nado’ wa Azam alioingia nao fainali katika mchakato wa tuzo za mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).,

 

Related Articles

Back to top button