
KLABU ya Namungo na kampuni ya Sportpesa zimesaini mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 1 na milioni 55 kuidhimi klabu hiyo kwa mwaka mmoja.
Namungo iko katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Agosti 15 ikifungua dimba dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa Majaliwa, mkoani Lindi.
“SportPesa imesaini rasmi mkataba mpya wa mwaka 1 wenye gharama ya TZS 1,055,000,000 wa kuendelea kuidhamini timu yetu ya Namungo FC,” imesema Namungo kupitia mitandao yake ya kijamii.
Sportpesa pia inazidhamini Yanga na Singida Fountain Gate.