Simba sasa ni ubingwa tu!

DAR ES SALAAM: UKISEMA Simba hii ubingwa washindwe wenyewe utakuwa sahihi kutokana na soka safi wanalolionesha huku wakipata ushindi wa maana katika michezo yao waliyokwisha kucheza mpaka sasa.
Wekundu hao wa Msimbazi wanatembeza tu vichapo kwa kila timu inayokatiza mbele yao hali inayowapa matumaini mashabiki wa Mnyama kwamba, msimu huu hakuna wa kuwazuia kutimiza malengo waliyojiwekea ya kutwaa ubingwa.
Mpaka sasa Simba wamepoteza mchezo mmoja peke na kutoka sare mchezo mmoja huku michezo mingine wakitoa dozi ikiwamo ushindi walioupata juzi wa mabao 5-2 dhidi ya Kagera Sugar.
Mchezo waliopoteza ni ule dhidi ya Watani zao wa jadi Yanga walipofungwa bao 1-0 lakini pia wakitoka sare mchezo mmoja dhidi ya Coastal Union wakifungana mabao 2-2.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema hakuna rangi wapinzani wao wataacha kuiona akianimi watatwaa ubingwa huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi mchezo wao wa kesho dhidi ya JKT Tanzania.
Ahmed amemaliza kwa kusema kwasasa viongozi wa timu hiyo wanafanyia kazi ripoti ya kocha wa timu hiyo ili kufikia malengo waliyojiwekea kwa pamoja.