Ligi KuuNyumbani

Ihefu, Namungo majaribuni tena leo

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa michezo miwili kupigwa Mbeya na Lindi.

Ihefu iliyopoteza mchezo wa ufunguzi kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Geita Gold ipo uwanja wa nyumbani wa Highland Estates, Mbarali mkoani Mbeya kuikabili Kagera Sugar.

Nayo KMC inayofungua kampeni ipo ugenini mkoani Lindi kuwavaa wenyeji Namungo ambayo ilipoteza mchezo wa ufunguzi mbele ya JKT Tanzania kwa bao1-0.

Related Articles

Back to top button