
BAADA ya kuirarua Vipers ya Uganda kwa goli 1-0 katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wekundu wa Msimbazi, Simba leo inashuka dimbani dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani mkoani Morogoro.
Simba ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 54 baada ya michezo 23 wakati Mtibwa Sugar unashika nafasi ya 9 ikikusanya alama 29 baad ya michezo 24.
Katika mchezo mwingine wa ligi leo Namungo itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.
Namungo inashika nafasi ya 7 ikiwa na alama 32 baada ya michezo 24 wakati Tanzania Prisons ipo nafasi ya 14 ikiwa na alama 22.