Ligi Daraja La Kwanza

“Tuko hapa kushinda mchezo” – Arteta

MADRID:KOCHA Mkuu wa Washika mitutu wa jiji la London Arsenal Mikel Arteta amesema safari yao mpaka Santiago Bernabeu jijini Madrid si utalii bali wapo jijini hapo kushinda mchezo na hatimaye kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ikiwezekana kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo.

Akizungumza na TNT Sports Arteta amesema wanawafahamu Real Madrid vyema na aina yao ya uchezaji hasa wanapokuwa kwenye Champions League na wamejiandaa vyema kuikabili hali yeyote itakayojitokeza na uwanjani Bernabeu.

“Sisi sio watalii Tupo hapa kushinda huu mchezo na hilo ndo jambo muhimu tutacheza kwa ujasiri na ‘mindset’ hiyo tutacheza kwa kujituma sana twende nusu fainali kwakweli tuna kazi ya ziada ya kufanya”

“Ni kama tupo ‘halftime’ wao (Real Madrid) pia wanaitafuta nafasi ya kuwa nusu fainali na ili iwe hivyo watapambana, tunajua tutakutana na nyakati ngumu, changamoto nyingi lakini halitatuondoa kwenye lengo letu la kuwa kwenye nusu fainali” – amesema Arteta

Arsenal walio na uongozi wa mabao 3-0 walioupata dimbani Emirates jijini London watakuwa na kibarua cha kulinda au kutanua uongozi huo mbele ya mabingwa watetezi Real Madrid katika mchezo ambao macho na masikio ya Dunia yataelekezwa huko hasa ukizingatia uhusiano mzuri wa Real Madrid na taji la UEFA Champions league. Swali ni je watatoboa?

Related Articles

Back to top button