Ligi Daraja La Kwanza

Polisi Tanzania yaandaa zawadi kwa mashabiki

KILIMANJARO: POLISI Tanzania imewahimiza mashabiki wake kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa Championship dhidi ya Songea United utakaochezwa Jumapili hii katika Uwanja wa Ushirika Moshi ikisema imewaandalia zawadi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ofisa habari wa timu ya Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kikosi hicho kipo imara na kinaendelea na maandalizi kabambe ya kuhakiksha kuwa wanafanya vizuri na kupata alama tatu muhimu ambazo zitakuwa zawadi kwa mashabiki wake.

“Mkoa wa Kilimanjaro una utamaduni wa kupokea wageni na wenyeji wengi kila mwisho wa mwaka hivyo tunawaomba waje kwa wingi ili waweze kupokea zawadi ya ushindi kwa kuwa tunajua shabiki ni mchezaji wa kumi na mbili uwanjani na tumejipanga kufanya vizuri katika mchezo tarajiwa” Amesema Lukwaro.

Amesema uongozi wa timu hiyo na wachezaji bado hawajakata tamaa katika kufikia malengo ya kucheza Ligi Kuu kama ilivyokuwa hapo awali ambapo ilikuwa tishio kutokana na kufanya vizuri kwa misimu mitatu ya mwanzo baada ya kutoka Ligi daraja la kwanza.

Mpaka sasa timu ya Polisi ipo nafasi ya 10 ikiwa na alama 13 baada ya kucheza michezo 12.

Related Articles

Back to top button