Mastaa

Aunty Ezekiel na Kusah wabarikiwa na mtoto wa pili wa kike

DAR ES SALAAM:MSANII maarufu wa filamu nchini, Aunty Ezekiel, pamoja na mume wake, msanii wa Bongo Fleva Salmin Ismail ‘Kusah’ wamepata mtoto wao wa pili baada ya Nono.

Mtoto huyo mpya ni wa kike, na amekuja kuongeza furaha ndani ya familia yao inayokua.

Kusah amethibitisha furaha hiyo akisema kuwa mtoto huyo ni wa kike, huku familia yao ikisherehekea kuzaliwa kwa mtoto huyo.

Kwa Aunty Ezekiel, huyu ni mtoto wake wa tatu, kwani mtoto wake wa kwanza, Cookie, alizaa na mpenzi wake wa zamani, Moses Iyobo.

Kwa upande wa Salmin Kusah, hii ni mara ya pili kuwa na mtoto baada ya kuwa na mtoto mmoja na msanii mwenzake Rubby.

Ingawa kulikuwa na kauli nyingi kuhusu mahusiano yao na wengine wakisema wasingeweza kudumu, sasa wameonesha umoja na nguvu katika familia yao, wakiwa sasa ni wazazi wa watoto wawili.

Wasanii na watu maarufu wengi wamewatumia pongezi kwa kupata mtoto wa pili, huku wakifurahi kwamba wote wanaendelea kuwa na afya njema.

Related Articles

Back to top button