Habari Mpya

Aucho haambiliki kwa Mbosso

DAR ES SALAAM: LICHA ya kuwa kiungo bora wa mpira, Khalid Aucho anayekipiga Yanga pia ni shabiki mkubwa wa muziki wa Tanzania.

Aucho amesema hata anapokuwa nje ya Tanzania huwa anasikiliza sana nyimbo za wasanii wa Tanzania lakini anapenda zaidi kusikiliza nyimbo za msanii Mbwana Yusufu maarufu Mbosso.

“Nasikiliza nyimbo nyingi nikiwa hapa Tanzania lakini pia nikiwa hata nje huwa nasikiliza lakini msanii wangu pendwa ni Mbosso nyimbo zake zinanivutia zaidi kuzisikiliza,” ameeleza

Aucho mwenye makazi yake nchini Misri amekiri kuwa shabiki wa Mbosso na kusema anapenda nyimbo zake zenye jumbe za kimapenzi na muziki wake unafika mbali.

Wasanii wengine wanaowasikilizwa zaidi na Aucho ni Nassib Abdul (Diamond Platinumz), Rajab Abdulkahal (Hamornize) na Omary Mwanga (Marioo).

Related Articles

Back to top button