Ligi Kuu

Ateba aja na moto ligi kuu

DAR ES SALAAM: WAKATI mashabiki na wadau wa Simba wakiwa na matumaini makubwa na mshambuliaji wao mpya, Leonel Ateba amesema ujio wake ni kuwapa changamoto washambiuliaji ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ateba ametambulishwa jana usiku kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea USM Alger ya Algeria ikiwa ni mapendekezo ya kocha Fadlu Davids akihitaji kuongezewa mshambuliaji.

Ateba ameahidi kuleta na matarajio ya pamoja na wachezaji wenzake, dhamira kubwa ni kufanya vizuri na anajianda kuandika ukurasa wake mpya ndani ya kikosi cha Simba.

“Najiandaa kuandika ukurasa wangu mwenyewe katika kitabu hiki cha hadithi chini ya rangi nyekundu na nyeupe, nawashukuru kwa dhati viongozi wa Simba kwa kuniamini hadi sasa ni motisha na ninajivunia kutowaangusha,” amesema mshambuliaji huyo ambaye anadai atakuwepo kwenye kikosi cha mchezo dhidi ya Tabora United.

Mshambuliaji huyo ameingia kambini na kuanza mazoezi rasmi kujiandaa na msimu mpya wa mashindano yaliyopo mbele yao ikiwemo Ligi Kuu, iliyoanza kutimua vumbi leo.

Related Articles

Back to top button