Tetesi

Arsenal kuachana na ESR

IMERIPOTIWA kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ana mpango wa kumuachia Emile Smith Rowe kwenda Leicester City ili kumnasa kiungo James Maddison wa klabu hiyo.

Arteta kwa sasa anakusudia kusuka upya kikosi hicho ambapo kwa mujibu wa ‘Football London’ wachezaji zaidi ya 10 wa timu hiyo wataachwa ili kusajili wengine ikiwemo wale waliotolewa kwa mikopo.

Arsenal imekuwa ikuhusishwa na Maddison kwa misimu miwili sasa, licha ya Leicester kuibania timu hiyo na kuamua kusalia na mchezaji wao.

Uamuzi wa kuachana na Rowe unakuja baada ya Arteta pengine kuona mchango wa Muingereza ni mdogo kwenye kikosi hicho kwa kuzingatia sio mchezaji tegemezi

Related Articles

Back to top button