Tetesi

Chelsea: Reece hauzwi bila Valverde

TETESI za usajili kutoka England zinasema klabu ya Chelsea itamuuza nahodha Reece James kwa Real Madrid iwapo tu itabadilishana na Federico Valverde. (Defensa Central)

Arsenal inawania saini ya beki wa kati wa Bayern Munich, Matthijs de Ligt lakini inahofu huenda dili likawa gumu kukamilika Januari 2024.(The Athletic)

Bayern inakusudia kuilipa Manchester United pauni milioni 17 ili kumsajili Raphael Varane, ambaye siku za hivi karibu hana nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza Old Trafford.(SPORT)

Conor Gallagher ni mmoja wa wachezaji watano wa Chelsea waliooneshwa mlango wa kutoka wakati wa dirisha dogo la usajili Januari 2024.(The Sun)

Tottenham Hotspurs imewaambia Eric Dier, Pierre-Emile Hojbjerg na golikipa Hugo Lloris kwamba wako huru kuondoka klabu hiyo Januari 2024.(Football Insider)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button