Tetesi

Enzo afikiria kuondoka Chelsea

TETESI za usajili zinasema kiungo wa Argentina Enzo Fernandez anafikiria kuondoa Chelsea mwaka mmoja tu baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa ada ya pauni mil 107 akisaini mkataba wa miaka nane na nusu. (FootballTransfers.com)

Wachezaji wa Chelsea wamelalamika kwamba ufundishaji wa kocha Mauricio Pochettino na benchi lake la ufundi ni wa kiwango kidogo huku wachezaji wapya wakieleza kujutia mikataba yao ya muda mrefu.(Athletic – subscription required)

Hata hivyo, Chelsea itasubiri hadi mwisho wa msimu kutathmini hatma ya Pochettino kama kocha.(Football.London)

Liverpool imewasiliana na kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso kufuatia uamuzi wa Jürgen Klopp kundoka Anfield mwisho wa msimu. (Footmercato – in French)

Paris Saint-Germain itafikiria uhamisho wa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, 26, iwapo itamuuza mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappé, 25, majira yajayo ya kiangazi. (CaughtOffside)

Vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England vina nia kumsajili beki wa Hispania chini ya miaka 17 anayekipiga Barcelona, Pau Cubarsi, ambaye ana kipengele cha kuachiwa cha pauni mil 8.5 katika mkataba wake.(ESPN)

Related Articles

Back to top button