KwinginekoTetesi

Hull City yamsajili Fabio Carvalho kwa mkopo

KLABU ya Championship huko England, Hull City imemsajili kwa mkopo winga wa Liverpool aliyekuwa akikiwasha kwa mkopo RB Leipzig, Fabio Carvalho hadi mwisho wa msimu huu.(BBC SPORT)

Tetesi za usajili zinasema Manchester United imejiunga na Newcastle katika mbio za kumsajili beki wa kati wa zamani wa Chelsea, Andreas Christensen kutoka Barcelona, ingawa Jean-Clair Todibo anabaki kuwa beki kipaumbele katika usajili wa United. (Football Insider)

Paris Saint-Germain inaangalia iwapo imsajili kiungo wa Bayern Munich Joshua Kimmich ambaye mkabata wake unamalizika 2025.(Sky Sports Germany)

Arsenal, Liverpool na Manchester United zote zinamfuatilia beki wa kushoto wa Bayer Leverkusen ambaye yupo kwenye kiwango bora Jeremie Frimpong. (Football Insider)

Related Articles

Back to top button