Ariana Grande: Nilijaribiwa kwa siri kuigiza kama mchawi
NEW YORK: MWANAMUZIKI Ariana Grande mwenye miaka 31 kabla ya kuigiza kama Glinda katika filamu mpya ya ‘Wicked’ amejaribiwa mara kadhaa kuigiza kama mchawi wa kijani wa Cynthia Erivo Elphaba katika filamu hiyo.
Muongozaji wa filamu hiyo inayotarajiwa kuachiwa katika majumba ya sinema nchini Marekani Novemba 22, 2024, Jon M. Chu amesema filamu hiyo inatokana na muziki wa Stephen Schwartz na inahusisha uhusiano wa wachawi wawili wachanga kabla haujavunjwa na Wizard of Oz, ambaye anatafuta mbuzi wa kafara ili kuondoa mawazo mabaya kutoka kwake.
Mtayarishaji huyo amefichua kwamba kabla ya Ariana kucheza kama Glinda alijaribiwa nafasi ya Elphaba nafasi ambayo inahusiana na mchawi wa kijani wa Cynthia Erivo Elphaba.
Katika mahojiano na Entertainment Weekly, Chu amesema: “Tulikuwa tukipokea ujumbe mseto. Bila shaka alikuja kwa ajili ya kucheza nafasi ya Glinda lakini mkurugenzi wangu aalitaka acheze nafasi ya Elphaba ambayo haikuwa mpango wetu,’
Ariana hivi majuzi amethibitisha kuwa amefanya majaribio ya sehemu zote mbili, hata kama alijua kwa siri alikusudiwa kucheza kama Glinda pekee.
Akiongea kwenye podikasti ya ‘Sentimental Man’, Ariana amesema: “Nilikuwa na ufahamu moyoni mwangu kila mara kwamba naenda kuwa Glinda, lakini nilikuwa nikisikia mambo mchanganyiko kutoka kwa watu ambao walikuwa wanataka nicheze kote.’
“Na nilidhani kwa kuwa hawakunijua walihisi ningeweza kumfahaa Elphaba! Nilijua kwa siri kwamba nilikusudiwa kucheza nafasi ya Glinda.”