Moto wa L.A waiteketeza nyumba ya mama wa Beyonce

MAMA Mzazi wa Msanii kutokea nchini Marekani Giselle Knowles ‘Beyonce’ anayejulikana kama Tina Knowles, ambaye ni mjasiliamali ametangaza kupoteza nyumba yake kutokana na moto mkubwa unaoendelea Los Angeles, Marekani
Kupitia video aliyoichapisha kwenye mitandao, Tina Knowles alionesha dondoo za samaki ‘dolphins’ wakielea katika bahari karibu na jumba lake la Malibu.
Alisikika akisema, “Hivi ndivyo nilikuwa nikivitazama kwenye siku ya kuzaliwa kwangu wikiendi hii iliyopita.”kisha akaongeza “Sasa imepotea.”
Alimshukuru Mungu na kuwatakia heri watoaji huduma za zima moto “Mungu awabariki wote wanaotoa huduma za janga la moto ambao walijitolea maisha yao katika hali hatarishi. Tunawashukuru kwa kujitolea kwenu na ujasiri wenu, na kwa kuokoa maisha mengi.”