Ancelotti haitaki kabisa Man City

BREST: Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema anatamani kukwepa kukutana na mabingwa watetezi wa ligi ya England Manchester city kwenye droo ya kesho ya michezo ya playoff ya ligi hiyo baada ya kikosi chake kukosa nafasi ya kufuzu moja kwa moja raundi ya 16 bora.
Ancelotti amesema hapendi kucheza dhidi ya Manchester City lakini ikitokea wamepangwa basi hana budi kucheza michezo hiyo ambayo itachezwa nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla kuungana na timu 8 zilizofuzu moja kwa moja.
“Ukweli ni kwamba sipendi kucheza dhidi ya City, lakini kama tutalazimika basi tutacheza kama tunavyocheza na wengine. Unajua Manchester City wana nafasi zaidi ya kushinda taji hili, lakini ni droo kinachokuja kinakuja kama unataka kushinda lazima ucheze kila mchezo na ushinde, tungeamka mapema tusingejipata hapa” – Amesema Ancelotti
Real Madrid huenda wakakutana na Celtic au Manchester City katika michezo hiyo ya playoff baada ya kukosa nafasi kwenye 8 bora waliofuzu kwa hatua hiyo moja kwa moja baada ya mwanzo mbaya wakipoteza michezo mitatu kati ya mitano ya mwanzo. Droo ya playoffs hizo itafanyika kesho Ijumaa Januari 31 mjini Nyon nchini Switzerland.